Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: shirika la habri la Novosti lanukuu: ripoti zinaonyesha kuweko na juhudi za kutaka kuuwa viongozi wa masuala ya ulinzi wa nchini Libya pia viongozi wa wajuu wa nchi hiyo, juhudi hizo zimeanza tarehe nne oktoba mwaka huu zikilenga kuangamiza viongozi wan chi hiyo
Kwamujibu wa ripoti hii mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha nchini Libya yamechukua sura mpya ya kukusudia kuuwa viongozi wakuu wa nchi hiyo ikiwemo baadhi ya wakuu wa jeshi la nchi hiyo katika mkoa wa Benghazi, ambapo siku iliopita kulitokea mapambano makli baina ya jeshi la Libya na wanamgambo hao nakupelekea kuuwawa wanajeshi kadhaa wa jeshi la Libya.
Pia katika ripoti hiyo shirika la habari hilo limeeleza kuwa makao makuu ya nchi hiyo Tripoli nako kumeonekana kunamapigano makali baina ya wanajeshi wa Libya na vikundi viliokuwa na silaha nchini humo, wananchi waliopo katika maeneo hayo wasema kuwa wanamgambo walio na silaha wameweza kumiliki vyombo vya habari vya mji mkuu huo na sasa wanauwezo wa kufanya kila kitu wanachokitaka katika maeneo hayo ya mkoa wa Benghazi na Tripoli.
6 Oktoba 2014 - 22:01
Msimbo wa Habari: 642659
Shirika la habari la Novosti limetangaza kuwa mkoa wa Benghazi nchini Libya katika masiku haya unaendelea kukosa Amani baada ya kuongezeka juhudi za wanamgambo wenye silaha nchini humo kutaka kuuwa viongozi na wakuu wa majeshi ya ulinzi nchini Libya